Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog

Wakenya zaidi ya 280 wakimbilia Tanzania

Katika kile kinachotanabaisha hali tete ya usalama nchini Kenya, raia zaidi ya 280 wameripotiwa kuikimbia nchi yao na kukimbilia Tanzania kutafuta hifadhi na fursa za kiuchumi kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na gazeti la 'Jamhuri, jumanne April 21-27',Wakenya hao wameingia kupitia Loliondo na Serengeti kwa nyakati tofauti.Imefahamika kuwa , mpaka sasa ni Wakenya 17 tu ambao wamekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kuingia nchini kinyume cha sheria.

Kufuatia tukio hilo, wito umetolewa kwa vyombo vya usalama kuimarisha ulinzi mipakani ili kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.Wachambuzi wa masuala ya usalama wanaonya kuhusu wimbi la kukithiri kwa matukio wa wahamiaji haramu nchini kama ishara ya kuteteleza kwa hali ya ulinzi mipakani.Hii ni kufuatia kukamatwa kwa genge la wahamiaji haranu mkoani Kilimanjaro mwezi uliopita pasi na kusahau kundi kubwa la wahamiaji haramu waliokamatwa katikati ya nchi mjini Dodoma huku wengine wakikutwa wamekufa na wengine wakiwa hoi.

Kwa vyovyote vile, Tanzania ni lazima ichukue tahadhari kuhusiana na wahamiaji haramu kwani vinginevyo huo waweza kuwa mwanya kwa makundi korofi ya kigaidi kupenyeza vibaraka wao

Tag(s) : #MATUKIO
Share this post
Repost0
To be informed of the latest articles, subscribe: