Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog

Majambazi wamefukua kaburi na kumwibia marehemu!

Katika hali inayoashiria kupungua kwa imani na ubinadamu nchini Tanzania, watu wanaosadikika kuwa majambazi wamefanya tukio la ajabu mno baada ya kufukua kaburi la marehemu na kuiba vitu kadhaa.

Tukio hilo limetokea aprili 24 mwaka huu katika eneo la mailimoja, wilayani Kibaha mkoani pwani.Majambazi hao walivamia kaburi la marehemu, walifukua na kumvua nguo zote marehemu kisha wakatoweka sambamba na mabegi aliyozikwa nayo.Imeelezwa kuwa kaburi hilo lilikuwa na mlinzi kwa siku za awali lakini mpaka tukio hilo linatendeka watu wamebaki midomo wazi.

Marehemu Napegwa Kishalula (75) alizikwa tarehe 20 april 2015 hivyo kaburi lake limefukuliwa siku nne tu baadaye.Haieleweki ikiwa majambazi hao hawaamini kuwa marehemu alistahili kupumzika pahala pema kaburini au lah.

Wengine wanahoji ikiwa ugumu wa maisha umefikia kiwango hiki, basi kuna haja ya kujitathmini upya kama taifa kuhusu mwenendo wa uchumi wetu maana huku ajali zimezidi, huku escrow, huku mauaji ya albino na kwingineko kuwaibia marehemu.

Itoshe tu kusema, Mungu awasemehe wahusika kwa maana siyo wajasiriamali bali hawajui walitendalo.

Tag(s) : #MATUKIO
Share this post
Repost0
To be informed of the latest articles, subscribe: