Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog

Katika kile kinachoonesha kuwa kampeni ya 'Learn without fear' haijakubalika miongoni mwa walimu wengi nchini, Mwanafunzi mmoja katika wilaya ya Kiteto mkoani Manyara alipigwa na walimu wake hadi kufa muda mfupi baadaye kwa kile kinachodaiwa kuwa alifeli mtihani wa kiswahili hapo juzi.

Mwanafunzi huyo wa shule ya sekondari ya Matui, kidato cha pili anadaiwa kupigwa na walimu watatu baada ya kupata alama 40 kinyume na makubaliano ya awali ambapo mkakati uliwekwa kuwa hakuna mwanafunzi anayetakiwa kupata alama chini ya 40.Polisi wilayani Kiteto wamekili kumshikilia mwalimu mmoja huku wengine wakikimbia.

Mkuu wa wilaya ya Kiteto, Kanali Samweli Nzoka alimtaja mwanafunzi huyo aliyepoteza maisha kuwa ni Noel Bichima.Baada ya tukio hilo wananchi waliandamana kuelekea katika kituo cha polisi Mtui.

Wakitoa maoni yao kwa hasira kal; wazazi wamekea tabia ya walimu ya kutumia nguvu kubwa katika kuwafundisha wanafunzi badala ya maarifa kama walivyofunzwa vyuoni.

Mwalimu wa kike akimwadhibu mwanafunzi

Mwalimu wa kike akimwadhibu mwanafunzi

Tag(s) : #Matukio
Share this post
Repost0
To be informed of the latest articles, subscribe: