Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog

Ushindi wa timu ya Bayern Munich ya Ujerumani dhidi ya FC Porto ya Ureno umetajwa kuwa ushindi wa kujihami kwa maana ya kufa au kupona kutokana na mazingira ya mechi yenyewe.

Alipokuwa akizungumza na kituo cha televisheni cha ZDF, kocha mkuu wa klabu ya Bayern Munich Meneja Pep Guardiola amesema, "kama ilivyokuwa kwa Barcelona, ilikuwa lazima tushinde ili tujitunzie heshima yet na tuzidi kusonga mbele katika michuano hii"

Katika mechi ya awali nchini Ureno, timu ya FC Porto iliutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani kwa kushinda 3-1 kabla ya kumiminiwa mvua ya magoli 6-1 katika mechi ya marudiano nchini Ujerumani katika uwanja wa Allianz Arena.

Mshambuliaji Robert Lewandowski alifunga magoli mawili na Thiago Alcantara, Jerome Boateng,Thomas Muller na Xabi Alonso pia walifunga goli moja moja.

Pep Guardiola akisherehekea ushindi sambamba na wachezaji wake

Pep Guardiola akisherehekea ushindi sambamba na wachezaji wake

Tag(s) : #Michezo
Share this post
Repost0
To be informed of the latest articles, subscribe: